NGUVU YA KWELI (NENO LA MUNGU)
Kweli ni uhakikiso wa jambo Fulani. Lakini kibiblia kweli
inajulikana kama “NENO LA MUNGU”. Maana biblia inasema kuwa “Uwatakase kwa ile
kweli; neno lako ndiyo kweli.”(Yohana 17:17).
Maisha ya wokovu kwa kila aliyemwamini KRISTO kuwa BWANA na
Mwokozi wa maisha yake, hubadilika na kulingana na jinsi huyu mwamini
anavyoishi kwa kuliaamini hili neno au anavyoishi kwa kuiamini hii kweli ya
neno la MUNGU. Hatuwezi kupata maendeleo
kimwili na kiroho, kama hatutaifahamu kweli ambayo inatakiwa kutuongoza kama
dira ya maisha maana Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu.
(ZABURI 119:105). Tukiifahamu kweli itatupelekea kuishi maisha ya ushindi
(victorious life).
ZIKO FAIDA ZA KUIFAHAMU KWELI
1) Tunapoifahamu
kweli inatuweka huru (Yohana8:32), inatuweka mbali na dhambi, mbali na utawala
wa mwovu ibilisi maana hapo mwanzo kabla ya kumwamini KRISTO tulikuwa chini ya
utawala wa Mungu wa Dunia hii yaani Ibilisi. Lakini kwa kifo cha msalaba cha
Yesu Kristo kilituletea ukombozi kutoka katika ufalme wa giza na tukahamishwa
kwenda kwenye ufalme wa mwana wa Pendo la Mungu yaani kwenye ufalme wa Nuru
(Wakolosai 1:13).
Mara nyingi unakuta mtu ameokoka lakini bado
mwasherati, kwa waganga anaenda, anavaa vimini (nguo zisizo za kusitiri),
kijana ananyoa viduku(Denge), anasengenya, anashiriki mizaa kama kawaida na
kusema uongo pia. Haya yote yanasababishwa na kutokuifahamu KWELI.
2)
Mwamini akiifahamu kweli Hasa kijana wa
kiume hataweza kunyoa kiduku(Denge) na kanisani hatutaweza kuwa na vijana
wanaonyoa viduku maana kunhyoa Denge ni dhambi (Walawi19:27). Haya yote
yanasababishwa na watumishi kutokuifundisha kweli kwa waumini.
3)
Hutakuwa mtu wa kutamani maana utafahamu
kuwa tamaa na uasherati ni dhambi mbele za Mungu na watu wa jinsi hii hawataurithi
ufalme wa Mungu (Wagalatia 5:19-21).
4)
Hutakuwa
mtu wa kuabudu sanamu maana ni dhambi (1Wakorintho 6:9), utajua kuwa
kuipenda dunia kuliko Mungu ni dhambi. Biblia inasema katika (1Yohana 2:15 ) “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo
katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.” Hii
inaonesha ni kwa jinsi gani tunatakiwa kumpenda Mungu kuliko kitu chochote kwa
mioyo yetu yote na kwa akili zetu zote (Mithali 3:5) “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe”.
Tusipomtumaini Mungu wetu na tusipomwabudu kama anavyotaka mwenyewe hapo
tutakuwa tunaabudu sanamu, yaani kutakuwa kuna kitu ambacho kinachukua nafasi
ya Mungu.
Lakini tukiifahamu
kweli hutajichanganya wala hutashindwa kumwabudu Mungu, utamwabudu Mngu kwa
viwango vya juu sana maana tuna ushirika naye yaani katika roho na kweli
(Yohana 4:23) .
5. Hutaogopa chochote wala
hutayaogopa mabaya yajayo juu yako maana Mungu amesema kwa neno lake kuwa
“usiogope, kwa maana mimi ni pamoja
nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguv,naam,
nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu” (Isaya 41:10). Lakini kwa sababu
ya kuikosa kwelindani ya moyo wako (mioyo yetu), unijukuta unaogopa wachawi,
majini, maadui zako n.k. Neno la Mungu huwa linatupa uhakika wa mambo yote
kwamba tufanye nini na Mungu anasema nini kuhusu kile tukionacho mbele zetu.
Na tunatakiwa kujua kuwa ukiwa
umempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, ndani yako panafanyika
kuwa makazi ya Yule MKUU katika
mambo yote yaani YESU KRISTO naye ni mkuu kuliko Yule adui ibilisi aliye katika
dunia hii (1Yohana 4:4).
6. Unapoifahamu kweli
magonjwa hayatakaa juu yako, wala hutakuwa tena chini ya laana ya magonjwa,
wala magonjwa hayatakutesa kwa sababu (Isaya 53:5) “Bali alijeruhiwa kwa makosa
yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi
tumepona”.
Hakika iko faida kubwa katika kuifahamu kweli ambapo hii kweli inatufanya tuwe na uhakika juu ya huyu Mungu katika kuufahamu zaidi uweza na nguvu zake zinavyotenda kazi katika maisha ya Mwanadamu.
Naye Mungu anasema ndiye atufundishaye tupate kuona faida.
Mungu akubariki mpendwa na akutie nguvu katika kuitafakari hii kweli ya Mungu.
BY. MWL. GEORGE JOHN
Comments
Post a Comment