Posts

Showing posts from June, 2017
UJUMBE WA KINABII KUHUSU KUNYAKULIWA KWA KANISA Kufuatia changamoto za kiimani ambazo jamii ya wanafunzi wa Yesu Kristo tunazipitia; na kutokana na matishio mbali mbali yanayotishia uhusiano wetu wa kiroho na Bwana Yesu; ni dhahiri kwamba umefika wakati wa kuzingatia vipaumbele vya imani ikiwa ni pamoja na kuzingatia ujumbe wa kinabii kuhusu kunyakuliwa kwa kanisa la Kristo. Mada hii inaanza kwa kuchambua maana ya misamiati wa kunyakuliwa, jinsi tukio litakavyokuwa, sababu za kunyakuliwa; na mchakato wa maandalizi ya unyakuo wenyewe. Karibuni. MAANA YA KUNYAKULIWA "Kunyakuliwa" ni tukio maalum la kinabii ambalo linatarajiwa kutokea wakati wowote kwa ajili ya kuhitimisha huduma za Kanisa la Kristo duniani. Tukio hili linawahusu makundi mawili ya walengwa. Kundi la kwanza ni “ kufufuliwa kwa wafu waliolala mauti katika Kristo ” ! Na kundi la pili ni “ wanafunzi halisi wa Yesu Kristo tutakaokutwa hai. Na hii ni kwa mujibu wa maandiko ya Paulo alipowaandikia ...
Image
NGUVU YA KWELI (NENO LA MUNGU) Kweli ni uhakikiso wa jambo Fulani. Lakini kibiblia kweli inajulikana kama “NENO LA MUNGU”. Maana biblia inasema kuwa “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”(Yohana 17:17). Maisha ya wokovu kwa kila aliyemwamini KRISTO kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yake, hubadilika na kulingana na jinsi huyu mwamini anavyoishi kwa kuliaamini hili neno au anavyoishi kwa kuiamini hii kweli ya neno la MUNGU.  Hatuwezi kupata maendeleo kimwili na kiroho, kama hatutaifahamu kweli ambayo inatakiwa kutuongoza kama dira ya maisha maana Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu. (ZABURI 119:105). Tukiifahamu kweli itatupelekea kuishi maisha ya ushindi (victorious life). ZIKO FAIDA ZA KUIFAHAMU KWELI 1)       Tunapoifahamu kweli inatuweka huru (Yohana8:32), inatuweka mbali na dhambi, mbali na utawala wa mwovu ibilisi maana hapo mwanzo kabla ya kumwamini KRISTO tulikuwa chini ya utawala wa Mungu wa Dunia hii yaani I...
Image